Posts

MIHULA YA MASOMO

  MIHULA YA MASOMO Shule yetu ina mihula miwili kwa mwaka kama ilivyo ratiba ya Wizara ya Elimu. Muhula wa kwanza huanza Januari na mwisho huisha Juni, na muhula wa pili huanza Julai hadi Disemba (Na kila muhula umegawanywa mara mbili ambayo ni robo ya kwanza na robo ya pili) Ada ya kila muhula hulipwa yote kila muhula unapoanza. Pia inaweza kulipwa kwa mwaka mzima.

TAALUMA

  TAALUMA Shule yetu ina waalimu waliobobea katika fani ya ufundishaji. Tumekuwa tukifanya vizuri miaka yote, na mitihani ya Darasa la saba 2021 tulifanya vizuri zaidi kiwilaya tulikuwa nafasi ya 25 kati ya shule 92. Kimkoa tulikuwa nafasi ya 134. kati ya shule 498, Kitaifa tulikuwa nafasi ya 518 kati ya shule 11,909.

USAFIRI

  USAFIRI Usafiri utalipwa kwa kila muhula na hii hutegemea na sehemu/umbali atokako mwanafunzi. Gharama zitabadilika kulingana na bei ya mafuta kwa wakati huo. Wazazi watakuwa wakijulishwa kuhusu badiliko lolote lile.

ADA

ADA Ada inalipwa kulingana na darasa ambalo mwanafunzi anasoma.

KUHUSU SISI

  KUHUSU SISI Anniy Nndumi Nursery and Primary School ni Shule ya Awali na Msingi, Kutwa na Bweni inayotumia lugha ya kingereza katika kufundishia Inatumia mitaala ya Wizara ya Elimu. Shule ipo katika Kata ya Saranga, Wilaya ya Ubungo, Mkoa wa Dar es Salaam. Shule ipo umbali wa kilometa tatu kutoka barabara kuu iendayo Morogoro mtaa wa Matangini mkabala na Shule ya Msingi Mavurunza

USAJILI

  USAJILI Tunapokea wanafunzi wa awali na msingi kwa wanaoanza na wanaohamia kutoka kwenye shule nyengine.

HUDUMA ZITOLEWAZO

HUDUMA ZITOLEWAZO Chai ya asubuhi na chakula cha mchana kwa wanafunzi wote. Usafiri wa uhakika kwa wote wanaohitaji huduma hii kwa vituol tulivyopanga. Mahitaji na huduma zingine muhimu kwa wanafunzi wote zinatolewa.